Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Hamid Maliki, Naibu Mkurugenzi wa Hawza ya Qum Iran, katika kongamano la makamishna na viongozi wa masuala ya wanafunzi na wahitimu wa hawza lililofanyika, Jumatano tarehe 14 Aban 1404 (5 Novemba 2025) katika ukumbi wa shule ya Ma‘sūmiyyah Qum Iran, alisema: “Katika historia yote ya Shia, fursa kama hii kwa hawza haijawahi kupatikana.” Adui amekasirishwa na nafasi ya leo ya wanazuoni wa dini
Naibu Mkurugenzi wa Hawza ya Qum aliongeza kusema: “Leo, taasisi ya wanazuoni wa dini imepata hadhi ambayo haijawahi kushuhudiwa. Adui amechukizwa vikali na jambo hili. Njama na kampeni za kuichafua sura ya uongofu wa kidini ni kwa sababu ya umuhimu wa nafasi hii.”
Akaendelea kusema: “Tunapaswa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutupa fursa hii kubwa. Huu ni wakati wa kufanya kazi usiku na mchana. Yeyote atakayepuuza majukumu yake leo, kesho hatakuwa na jibu la kutoa mbele ya Mungu.”
Akiashiria njama pana za maadui katika kuudhoofisha uwanja wa imani, alisema: “Maadui walikuwa wamepanga kwa miaka mingi mapambano haya. Wamewafuatilia watu katika taasisi mbalimbali, wakawashawishi kwa tamaa, na wakatayarisha vibaraka watakaotekeleza mipango yao kwa wakati ufaao. Hata hivyo, licha ya njama zote hizi, wanazuoni wa dini lazima wabaki macho, wapigane kwa juhudi, na watimize jukumu lao la kihistoria.”
Wanafunzi wa dini wajione kuwa wanadeni kutoka kwa Imam Mahdi (a.t.f.s.)
Hujjatul-Islam Maliki alisisitiza: “Leo ni uwanja wa huduma na msaada. Tunapaswa sisi wenyewe pamoja na wanafunzi wa dini tujitengeneze kimaadili na kiimani kiasi kwamba kila mmoja ajihisi anadaiwa na Imam wa zama (a.j.). Hisia hii ya uwajibikaji ndiyo siri ya uimara na mafanikio ya hawza.”
Hawza ndio mfasiri wa mwenendo wa Ahlul-Bayt (a.s.)
Akiashiria nafasi ya kimkakati ya hawza, alisema: “Hawza ni mfasiri wa mfumo wa maisha na mwenendo wa Ahlul-Bayt (a.s.). Wanafunzi wa dini lazima watambue thamani ya nafasi hii na kwa unyenyekevu, ikhlasi na uaminifu, watimize wajibu wao katika kubainisha mafundisho ya dini na kuwahudumia watu.”
Kuwahudumia askari wa Imam Mahdi (a.j.) ni jukumu kubwa
Mwalimu huyo wa Hawza ya Qum aliendelea kusema: “Kuwahudumia askari wa Imam Mahdi (a.j.) ni jukumu kubwa; kwa hakika ni sawa na kuihudumia dini yenyewe. Kwa hiyo, yeyote anayechukua hatua katika njia hii, kwa hakika anachangia katika kuiimarisha dini ya Uislamu. Kwa msingi huu, nafasi yenu katika kuyaendea masuala ya wanafunzi ni ya umuhimu mkubwa sana.”
Vazi la wanazuoni ni vazi la kuuhudumia kwa Uislamu
Mwisho, Naibu Mkurugenzi wa Hawza ya Qum, akitoa shukrani zake kutokana na juhudi za viongozi wa masuala ya wanafunzi na wahitimu wa hawza, alisema: “Wanafunzi wa dini na wanazuoni lazima watambue kwamba; daima kwamba vazi hili ni vazi la kuuhudumia Uislamu. Tambueni thamani ya nafasi hii na majukumu makubwa mliyopewa.”
Maoni yako